Waziri Masha alizwa
SERIKALI kupitia Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imeteua kampuni sita zitakazoingia katika mchakato wa kupata kampuni moja itakayopewa kazi ya kuandaa mfumo wa vitambulisho vya taifa, huku Kampuni ya Sagem Securite iliyokuwa ikipigiwa chapuo na Waziri Lawrence Masha, ikitupwa nje.
Kampuni hizo ambazo zitaendelea kuchujwa ili kupata kampuni moja itakayopewa kazi ya kuandaa vitambulisho hivyo zimepatikana baada ya mchujo wa kwanza ulioshirikisha kampuni 54 ambazo zilituma maombi ya zabuni hiyo.
Katika kampuni hizo sita zilizoshinda hatua ya awali, tatu zinatoka nchini India, moja Afrika Kusini, Malaysia na Japan.
Taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Wizara hiyo, Isaac Nantanga, ilizitaja kampuni zilizoteuliwa na nchi zinakotoka kwenye mabano kuwa ni Unisys (Afrika Kusini), Giesecke & Devrient Fze (India), Iris Corporation Berhad (Malaysia) na Madras Security Printers (India)
Nyingine ni Marubeni Corporation ikishirikiana na Zetes pamoja na Nec (Japan) na Tata Consultancy Services ambayo inashirikiana na Ontrack Innovations Ltd (India).
Mchujo wa pili ambao utahusisha kampuni hizo, unatarajia kuanza mara moja na kukamilika haraka iwezekanavyo ili mradi huo uanze haraka.
Hata hivyo taarifa hiyo si nzuri kwa Waziri Masha, kwani alijitokeza kuitetea Kampuni ya Sagem Securite, kupinga kuenguliwa kwake, kwa madai kuwa ina uwezo wa kuendesha mradi huo.
Akizungumzia hatua hiyo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, alisema kuwa Waziri Masha anapaswa kujiuzulu kwani hoja yake imeshindwa....bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment