Baba ziro mtoto sifuri
Baba mmoja alikuwa akimchapa mwanae kwa kosa la kutofanya vizuri kwenye mtihani, mara mkewe akatokea na mazungumzo yalikuwa hivi:
Mke: Jamani mume wangu mbona unampiga mtoto kiasi hiki nhe?
Mume: Hana akili kabisa huyu
Mke: Kwani kafanyaje?
Mume: Kakosa swali rahisi sana kwenye mtihani ananitia aibu
Mke: Swali gani?
Mume: Eti hamjui Rais wa Zanzibar ni yupi
Mke: Yeye kajibuje?
Mume: Eti kajibu Rais ni Lipumba wakati Rais wa Zanzibar ni Mrema
Mke: Ebo! We ziro na mtoto pia sifuri...
Toka Global Publishers TZ.
No comments:
Post a Comment