
Kwa nini wanaume
wanatunyamazisha na misuli,
kwani misuli ni akili?
Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
Mpenzi Frank,
BILA shaka mu wazima si wazimu kama wengine. Vipi mihangaiko huko?
Nilitarajia utanitakia heri ya siku ya wanawake angalau, lakini kimyaaa! Au utaanza mambo zako za kudai mwanamume awe na siku yake pia. Hujui kwamba wanaume wana siku 364, iweje mtuonee gere kwa hii siku moja tu?
Hata hivyo, naona siku hii ni kwa ajili ya walio nacho. Nani anatukumbuka sisi wafanyakazi wa ndani siku hiyo? Kila mara ni mambo ya kuongeza nafasi za uongozi kwenye ngazi za juu, na mengine kama hayo. Mimi na wenzangu …. Aaaah! Ingawa hapo si tofauti na wanaume pia. Waheshimiwa na vitambi vyao watakumbuka akina Frank mwaka gani kama si wakati wa kutafuta kura zao kwa nguvu zote?....bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment