Monday, April 27, 2009

Bombo la nguruwe

laingia Norway.

Mtu mmoja alazwa

mjini Haugesund


Virusi vya bombo la nguruwe (swine influenza virus) vimeingia Norway. Mgonjwa mmoja amelazwa kwenye hospitali ya Haugesund (Norway), linaripoti gazeti la VG mtandaoni. Mgonjwa huyo ametoka safarini Houston, Texas nchini Marekani. Vipimo vya mgonjwa huyo vimeletwa Oslo, kwenye idara ya afya ”Folkehelseinstittutet”.

Bombo la nguruwe linaweza kuambukizwa toka kwa nguruwe hadi kwa binadamu na kutoka kwa binadamu hadi kwa binadamu mwingine, kwa kukohoa, kupiga chafya au hata kukaa karibu na mgonjwa.

Bofya na soma kiungo hiki.

No comments: