Picha ya keki ya harusi
yawasaliti. Wagunduliwa
si wakimbizi kama
walivyodai!!!
Hii ndiyo picha ya harusi yao.
Historia inaanzia kwa mwanamke mwingine aliyekuja kuomba ukimbizi kabla yao na kukataliwa halafu akaenda Ujerumani.
Mwanamke mmoja kutoka Burundi alikuja Norway mwaka 2000 na kuomba hifadhi ya kikimbizi, akakataliwa. Mwaka 2003, mwanamke huyo alienda Ujerumani na kuolewa na Mjerumani.
Kaka wa huyo mwanamke alipata viza toka Burundi kwenda Ujerumani kuhudhuria harusi ya dada yake. Baada ya harusi, huyo jamaa akaja Norway na kuomba ukimbizi kwa kudanganya! Jamaa akapewa kibali cha hifadhi ya kikimbizi. Baada ya miaka miwili, mkewe akaja Norway bila ya kitambulisho cha aina yoyote, wala pasipoti. Kwenye mahojiano ya kuomba ukumbizi, mwanamke huyo, alidai kuwa alikamatwa na moja ya kikundi cha wanamgambo nchini Burundi na kufichwa msituni kwa miaka miwili. Katika kipindi hicho cha miaka miwili, huyo mwanamke akiwaeleza polisi wa uhamiaji kuwa, alikuwa akifanywa mtumwa wa ngono na hao wanamgambo.
Baada ya miaka mitatu, kesi ya huyo mwanamme na mkewe, ikaangukia kwenye kitengo cha polisi kinachoshughulikia uhamiaji wa wageni (Politiets utlendingsenhet). Polisi wakaiomba mahakama na kupata ruhusa ya kupekua nyumba yao. Polisi wakakuta albam la picha za harusi za mwaka 2003 hadi 2005 (miaka ambayo huyo mwanamke alidai alikuwa mtumwa wa ngono) kati ya huyo jamaa na huyo mwanamke. Polisi wakaikuza hiyo picha ya harusi, na kuona majina yao na mwaka kwenye keki ya harusi!!!
Picha ya harusi imewasaliti. Jamaa hawakuwa walalahoi huko Burundi kama walivyodai walipokua kuomba ukimbizi.
Polisi wameiomba mahakama iwafukuze mtu na mkewe.
No comments:
Post a Comment