Thursday, April 16, 2009

Wakiona hata kivuli cha

ukombozi wanakikimbiza

hadi viatu vinakatika



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo. 

 

Mpenzi Frank,

VIPI hali yako ya kubangaiza siku hadi siku.  Ule mkopo wa kikundi umekwisha kuupata au  bado wanakuzungusha zungusha?  Sidhani hata wanene wanatutakia mema sisi vijana hata wakiahidi mabilioni.   

Mbona mabilioni hatuyaoni? 

Lakini nashukuru umekataa huu mpango wa tajirika haraka.  Labda tungesikia mwanzoni maana katika mambo hayo ujanja kuwahi. 

Sasa waliowahi wanastareeeehe na nyumba zao na nini sijui, hawa wote wanaojipeleka sasa watavuna kweli huku wamepanda ndani ya shamba ambalo ardhi yake imechoka kabisa? … bofya na endelea>>>>>


No comments: