Friday, June 12, 2009

Hayawi hayawi huwa!

C. Ronaldo aondoka

Old Trafford atua

Santiago Bernabéu

Hatimaye Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro,ameamua kuondoka Manchester United na kuelekea Real Madrid Club de Fútbol. Kuondoka kwa Ronaldo toka Old Trafford kuelekea Santiago Bernabéu, kumekuwa kukitabiriwa na wapenzi wa soka kwa muda mrefu sasa. Mara ya mwisho baada ya fainali za UEFA Champion League, Ronaldo alipomkandia kocha mkuu wa ManU, Sir Alex Ferguson kwa mbinu alizotumia kwenye fainali hizo kusababisha Manchester United kufungwa na Barcelona.


Real Madrid timu yenye mafanikio makubwa Ulaya na labda duniani, imewahi kushinda ligi kuu ya Hispania (La Liga) mara thelathini na moja, Kikapu cha Hispania mara kumi na saba. Mara saba imeshinda UEFA Champion League na mara mbili UEFA Cups. Uwanja wao ni Santiago Bernabéu, wenye kuchukua watu 90.000. Na ambako patafanyika fainali za UEFA Champion League mwaka 2010.

Real Madrid wanamsaini Ronaldo kwa Paundi milioni 80 (Shilingi za Kitanzania 173.200.000.000/= au Kroner za Kinorwejiani milioni 825). Hii inavunja rekodi zote duniani za mchezaji wa soka kununuliwa toka klabu hadi ingine kwa kiasi kikubwa kama hicho. Rekodi ya zamani ilikuwa inashikiliwa na Zinedine Zidane aliponunuliwa na hao hao Real Madrid.

No comments: