Thursday, June 11, 2009

Gaddafi yuko nchini Italia.

Apiga hema lake la Kibedui

nje ya hoteli.


Colonel Muammar Abu Minyar al-Gaddafi

Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi ameanza ziara yake ya kwanza nchini Italia kwa kupokewa na mwenyeji wake waziri mkuu Silvio Berlusconi. Gaddafi akiandamana na walinzi wake wa kike, The Amazon na wajumbe wengine wa msafara, amepiga hema nje ya hoteli aliyofikia.

Mapokeza mazuri aliyoyapata ni ishara ya kuwapo mahusiano mazuri kati ya taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa nishati na mtawala wake wa kikoloni Italia.

Ziara ya Gaddafi ya siku nne itakuwa ni pamoja na hotuba , pamoja na heshima adimu ya kulihutubia baraza la seneti la Italia.

Pia amekubali kukutana na baadhi ya Wataliani 20,000 ambao aliwafukuza mwaka 1970 katika hatua ya kuiadhibu Italia kwa utawala wake wa kikoloni kuanzia 1911 hadi 1947.

Shirika la kutetea haki za binadamu linalaumu ziara hiyo , likisema kuwa inakamilisha makubaliano haramu yaliyofikiwa hivi karibuni ambapo Italia inawarejesha nchini Libya wahamiaji haramu waliookolewa baharini.


No comments: