Tuesday, June 30, 2009

Tanzania:

Uuzaji holela kadi za

simu kukoma


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA

USAJILI WA SIMU ZA MKONONI





Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communications Regulatory Authority = TCRA) inawajulisha wananchi kuwa kuanzia tarehe 1 Julai 2009 makampuni yote ya simu za mikononi yataanza kusajili wateja wao waliopo na wapya ili kuhakiki umiliki wa namba za simu wanazozitumia. Zoezi hili litaendelea kwa miezi sita hadi tarehe 31 Desemba 2009.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inawahimiza wananchi kufahamu na kuzingatia mambo yafuatayo ambavo yametayarishwa kwa mfumo wa maswali na majibu.

1. Swali: Kwa nini usajili namba ya simu?

Jibu: Kwa ajili ya kukulinda wewe na namba yako dhidhi ya matumizi mabaya ya simu.

2. Swali: Kitambulisho cha aina gani kitahitajika wakati wa usajili?

Jibu: Ili uweze kusajiliwa unahitaji kufika kwenye ofisi ya kampuni yako ya simu au wakala wake na moja ya vitambulisho vifuatavyo ambapo utawapatia kivuli chake:-

(i) Kitambulisho cha mpiga kura

(ii) Pasipoti

(iii) Kitambulisho cha mfuko wa pensheni

(iv) Leseni ya udereva

(v) Kitambulisho cha SACCOS

(vi) Kitambulisho cha benki

(vii) Kitambulisho cha ajira pamoja na barua ya mwajiri

(viii) Kitambulisho cha chuo cha elimu ya juu

(ix) Kitambulisho cha uanachama kwenye kilabu

(x) Barua ya serikali za mitaa ikiwa na picha, sahihi na muhuri.

3. Swali: Nisipojisajili ifikapo tarehe 31Desemba, 2009 nini kitatokea?

Jibu: Namba yako itafungwa ili usiweze kuitumia kwenye mtandao wa simu nchini

Tanzania.

4. Swali: Nani na wapi ninaweza kusajili namba yangu ya simu?

Jibu: Unaweza kusajiliwa na kampuni yako ya simu za mkononi au mawakala wao waliopo sehemu mbali mbali nchini.

5. Swali: namba ngapi za simu (simcard) ambazo ninaweza/ninaruhusiwa kusajili?

Jibu: Idadi yoyote kadri utakavyo.

6. Swali: Kuna uhakika gani wa usiri wa taarifa zangu nitakazotoa kwa kampuni ya simu za mkononi au wakala wao?

Jibu: Kampuni zote za simu nchini zinawajibika kwa mujibu wa sheria, kutunza taarifa za wateja wao ikiwa ni pamoja na taarifa za matumizi.

7. Swali: Taarifa zipi zinahitajika wakati wa usajili?

Jibu: Tafadhali angalia mfaano wa fomuya usajili hapo chini:-

Imetolewa na

Mkurugenzi Mkuu

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Bofya na angalia fomu ya usajili.


2 comments:

Jamaldeen T. Bin Mazar E Shariff Ibn Zenjibari said...

Hili zoezi lingekuwa rahisi kama rais wote wa Tanzania na wote raia wa nchizingine wanaoishi Tanzania wangekuwa computerized kwenye database. habari binafsi za mtu zinajitokeza kwenye screen ukigonga national identity number...haya ya kujaza makaratasi kila siku...hayatatufikisha mbali. Watu kuwa kwenye database kunarahisisha mengi mno...tungekuwa hatuhitaji hata sensa ya taifa ya kila baada ya miaka kumi. Mtu akizaliwa automatiki anaingia kwenye database. Anayekufa automatic anatolewa kwenye database. Ukiomba pasi...jamaa wa uhamiaji wanagongwa namba zako, puuu unaonekana. Ukihama unatoa taarifa kwenye "idara ya sensa" unahamishwa automatic. hata kwenye chaguzi inakuwa rahisi...ulalamishi unakuwa mdogo kuwa oooh...jamaa wameingiza majiana yasiyokuwepo unakuwa haupo!!!! n.k.Urasimu unapungua.

Kwa maoni yangu: Serikali ingefanya mkakati wa kuwaingia raia wake kwenye database kwanza...

Jamaldeen T. Bin Mazar E Shariff Ibn Zenjibari said...

Ilikuwa isome kama "raia wote" badala ya "rais wote"