Friday, June 12, 2009

Leo ni uchaguzi Mkuu

nchini Iran. Nani ataibuka

mshindi? Vigumu kutabiri!


Rais wa Iran, Mahmoud Ahmedinejad


Waziri mkuu wa zamani Mirhossein Mousavi.


Wagombea wa uchaguzi wa rais nchini Iran wamemaliza kampeni zao kali jana, ambapo wanaopendelea mageuzi wanamatumaini kuwa uchaguzi huo utamzuia rais mwenye msimamo mkali Mahmoud Ahmedinejad kushinda kipindi kingine cha pili.

Kampeni hizo zimekuwa kwa kiasi kikubwa na hali ya kupakana matope kisiasa pamoja na maandamano makubwa mjini Tehran yaliyofanywa na waungaji mkono waziri mkuu wa zamani mwenye msimamo wa kati Mirhossein Mousavi.

Uchaguzi unafanyika leo Ijumaa unaweza kuelekeza hali ya uhusiano kati ya Iran na mataifa ya magharibi , ambayo yana wasi wasi na shughuli zake za kinuklia, na wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa ushindi kwa Mousavi unaweza kuongeza matarajio ya uwekezaji wa mataifa ya magharibi katika taifa hilo la Kiislamu.

No comments: