Friday, June 12, 2009

Mfalme naye

kachunguliwa mawasiliano

yake ya mtandaoni?



Mfalme Harald wa Norway.

Inasadikiwa kuwa Kasri (Hekalu) la Mfalme Harald nalo limechunguliwa mawasiliano yake ya mtandaoni na idara ya usalama jeshini, FOST (Forsvarets sikkerhetstjeneste). ”Ni kweli kunafanyika uchunguzi wa tuhuma hizo, zaidi ya hapo siwezi kusema lolote, ni kweli kumekuwa na mawasiliano kati ya Kasri la Mfalme, wizara ya ulinzi na Kripos.” msemaji wa Kasri la Mfalme, Bw. Sven Gj. Gjeruldsen alisema.

Kama FOST watabainika kuwa wamekuwa wakichungulia mawasiliano kwenye Kasri la Mfalme, itakuwa ni skendo kubwa hapa Norway. FOST watakuwa wamevuka mipaka ya majukumu yao ya kazi. Moja ya kazi ya FOST ni kulinda mawasiliano ya TEKNOHAMA (TEKNOlojia ya HAbari na MAwasiliano) kwenye kasri la mfalme na familia ya Kifalme, yasiingiliwe na watu wasiohusika. Endapo wakigundua kuna kasoro, wanapaswa kutoa taarifa kwenye Idara ya usalama wa taifa, PST (Politiets sikkerhetstjeneste) ambao ndio wanapaswa kuchukua hatua zaidi, na si kuchungulia nini kinafanyika ndani ya mawasiliano kama ambavyo wamefanya.


No comments: