Wednesday, July 01, 2009

Kuanguka kwa Yemenia:

Mtoto wa kike wa miaka 14

ndiye pekee aliyepona!!!




Yemanias Aibus 310.



Ajali ya ndege ya shirika la ndege la Yemenia (la Yemen) iliyotokea jana asubuhi kwenye bahari ya Hindi karibu na Moroni, Komoro; imetoa maajabu. Mtoto wa kike wa miaka 14, Bahia Bakari anayeishi Marseille nchini Ufaransa, kimaajabu ndiye aliyepona kwenye ajali hiyo. Bahaia aliogelea miongoni mwa maiti na mabaki ya ndege aliwashangaza waokoaji, Radio Europe 1 France, inanukuhu waokoaji hao.

Ndege hiyo ya Yemenia iliyoanguka jana, ilipata matatizo miaka miwili iliyopita, na mamlaka ya usafiri wa anga ya Ufaransa ilitoa onyo kwa shirika la ndege la Yemenia. Hata hivyo, waziri wa usafiri wa Ufaransa Dominique Dosserreau amesema kuwa ndege hiyo haikuwahi kurudi nchini Ufaransa toka ilipopata matatizo.

Chombo maalumu “Black Box” cha kurekodi nyendo za ndege, kimepatikana.


No comments: