imefika mwisho
General Motors (GM) ya Marekani inayomiliki kampuni ya SAAB ya Sweden, imefikia uamuzi wa kufunga kiwanda kinachoteneneza magari ya SAAB. GM imetengaza jana Ijumaa.
Hali ya uchumi na kifedha ya SAAB imekuwa mbaya muda mrefu, mpaka GM ikachukua hisa kubwa na kumiliki kampuni hiyo.
Hali ya kiuchumi ya SAAB ilizidi kuwa mbaya zaidi, baada ya mgogoro wa kifedha ulipoanza mwaka jana. GM imekuwa na mazungumzo na Koenigsegg kuhusu kununua SAAB, mazungumzo hayo hayakufikia kokote baada ya kushindwa kuafikiana. Juzi juzi, Spyker Cars ya Uholanzi, ilifanya mazungumzo na GM, lakini hawakufikia makubaliano.
Kampuni ya Beijing Automobile Industry Holding Corp. (BAIC) imenunua hakimiliki za baadhi ya injini na magari ya SAAB ili kutengeneza aina ya magari tofauti na ya SAAB.
Chanzo: Svenska Dagbladet.
No comments:
Post a Comment