Friday, December 11, 2009

Ujio wa Obama mjini Oslo

Polisi wavunja na kuingia

ndani ya nyumbani bila

ya idhini



Familia ya Kisomali: Mama Nimco Karse (38), Deca (12), Sabrin (3), Said (9), Samaya (11) wakiwa nyumbani kwao karibu na ubalozi wa Marekani mjini Oslo.


Juzi Alhamisi, polisi walivamia nyumba ya familia hiyo hapo juu wakavunja mlango wa nyumba, wakaingia na kuangalia ndani. Baada ya kufanya ukaguzi ndani ya ”fleti”, wakafunga madirisha na kubadili mlango bila idhini ya mwenye nyumba ya mama mmoja wa Kisomali, Nimco Karse. Wakati wakifanya yote hayo, familia hiyo haikuwa nyumbani. Binti wa mama huyo, Samaya aliporudi nyumbani akajaribu kufungua mlango ikashindikana. Mlangoni kuliwa na maandishi –

”Kwa sababu madirisha yalikuwa wazi na mapazia yamefungwa, polisi ilibidi kuingia ndani na kuangalia. Njooni polisi mchukue funguo mpya”

Samaya hana simu ya mkononi, hivyo ilibidi akae nje amsubiri mpaka mama yake aliporudi toka kazini. Mama naye aliporudi ikabidi awasubiri watoto wake wengine waliokuwa bado wako shuleni mpaka waliporudi.

Mama wa watu hakuweza kwenda polisi, hivyo aliwapigia na polisi wakamletea funguo mpya. Msemaji wa polisi wa Oslo, Bi. Unni Grøndal alipoulizwa juu ya tukio hilo, alijibu kuwa ilikuwa ni lazima kwa sababu za tahadhari za kiusalama kufuatia ujio wa Rais Obama mjini Oslo.

Wakazi wa maeneo ya karibu na ubalozi wa Marekani ambao hauko mbali na taasisi ya Nobel, na maeneo ya karibu ya hoteli ya Grand alikofikia Obama, walipewa taarifa siku nyingi kuwa wasifungue madirisha wala kuchungulia madirishani siku Obama atakazokuwa Oslo.

No comments: