Wanafunzi UDSM kuishtaki
serikali. Wataka kiswahili
serikali. Wataka kiswahili
kiwe lugha ya kufundishia.
Wanafunzi wa shahada ya Uzamili - Kiswahili wa Chuo Kikuu cha Dar wapo mbioni kufungua kesi ya kikatiba katika mahakama kuu dhidi ya Serikali ya Tanzania kwa kuzuia uhuru wa kutoa maoni/kujieleza kwa Watanzania kwa kuruhusu Watanzania wajieleze kwa lugha ya Kiingereza, na dhidi ya sera onezi ya lugha mwigo wa ukoloni.
PIA WANADAI + KUSEMA + KULAANI:
Wanasema kuwa hakuna Nchi duniani iliyoweza kuendelea kwa lugha za watu wengine.
Wanalaani mauaji ya halaiki ya watoto wa Kitanzania katika fikra zao kwa kusoma katika mazingira yao kwa lugha za wakoloni/wageni.
Wanalaani viongozi wenye mamlaka makubwa ya kisera kuutukuza ukoloni mkongwe na vipamba ukoloni mkongwe huo ikiwemo lugha, mintaarafu lugha ya Kiingereza.
Wanazidi kusubiri na kukumbushia ahadi ya Waziri Mkuu aliyoitia mwezi wa saba UDSM kwenye ufunguzi wa TATAKI (IKS) kuwa lugha ya Kiswahili itumike kama chombo cha kufundishia.
Wanaalani sana kuwa ni sawa na watu waliotupwa katika kisiwa ombwe- kifikra, hivyo kukosa utamaduni wao madhubuti na kitambulisho chao sahihi katika uwanja wa Taifa na kimataifa.
Wanasema - China, Urusi, Uturuki, Sweden, Uingereza, Norway, Ubelgiji wameendelea kwa lugha zao wenyewe.
Wanakubali umilisi na umahiri wa lugha ya Kiingereza kwa watanzania kama lugha yoyote ya ujuzi na utambuzi zaidi, lakini isiwe lugha ya ukuzaji wa fikra pembuzi kwa Watanzania.
Wanadai kuwa maamuzi haya yatapelekea kujuta na kusababisha kifungo cha roho kitakachoplekea kuwa omba omba siku zote kama hali hii inavyoongezeka siku hadi siku kwa Watanzania.
Fikra bebuzi hutokana na ujuzi wa lugha mama, uletao maendeleo ya kiuchumi.
No comments:
Post a Comment