Hakikisha unakwangua
theluji/barafu gari yako,
unaweza kujuta!
Polisi wa usalama barabarani wamechoshwa na madereva ambao huendesha magari yao bila ya kukwangua theluji/barafu vizuri kwenye magari yao. Ukikutana nao matrafiki huku vioo vya gari yako vimejaa theluji/barafu unaweza kupigwa faini ya kuanzia kroner 2000,- hadi kroner 18000,- Unaweza kupoteza leseni kwa miezi mitatu kama kioo cha mbele kimejaa theluji. Jamaa mmoja mkoa wa Buskerud (bofya angalia) amenyang´anywa leseni yake kwa miezi mitatu, baada ya kukamatwa huku kioo cha mbele kina theluji.

No comments:
Post a Comment