Monday, February 22, 2010

Unatumia iPhone?




Unaweza kufyonza (download) Kamusi Elezo (Kiswahili).

Kwenye "Apps Store" halafu ”search” andika Kiswahili, halafu unafyonza. Inagharimu Kroner 35,- (thelathininatano). Lakini ni nzuri kwa
marejeo (references):

Mfano: Nimetafuta “Kariakoo”

Kariakoo: ni jina la kata ya Wilaya ya Ilala katika mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania. Kariakoo inajulikana kutokana na soko kubwa.


Jina la eneo hili ni la kihistoria linatokana na neon la Kiingereza “carrier corps” yaani kikosi cha wapangaji waliobeba mizigo ya jeshi wakati Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia...........

3 comments:

Anonymous said...

Hivi iPhone ina madubwana yepi? Manaake kila mwenye iPhone anaonekana kuipenda kuliko vidubwana vingine vya TEKNOHAMA...

Mosi-O-Tunya said...

Eeeeh Bwana eeeh usisikie ndugu yangu...

iPhone kiboko yao.

Zingine zote zinaiga toka iPhone.

Apple waliposhusha iPhone ilikuwa ni tetemeko la ardhi kwenye TEKNOHAMA.

Huwezi kujua "utamu" wake mpaka uwe nayo. Ukiwa nayo ndipo utaelewa iPhone ni nini.

Nasubiri kakake iPhone yaani iPad akitoka madukani, nitakuwa wa kwanza kupanga foleni, hata ikiwa nitalala nje kwenye theluji. Siku moja sitokufa.

Kaziyabure said...

Baab Kubwa