Breki zimegoma
Kilomita 176 kwa saa!
Toyota Prius 2010
Jamaa mmoja (41) akiendesha Toyota Prius kwenye E18 (European Highway no.18) kuelekea Lillesand, alipatwa na mshtuko wa mwaka baada ya breki za gari yake kuacha kufanya kazi akiwa kwenye kasi ya kilomita 176 kwa saa. Tukio lilitokea jana Alhamisi saa 12:26 CET, anaripoti Petter Osaland wa polisi Agder mkoa wa Rogaland. Jamaa huyo aliwapigia polisi kwa kutumia simu ya kiganja, polisi nao wakawapigia Toyota ili wawape maelekezo ya jinsi ya kumsaidia jamaa kusimama.
Polisi walipompigia jamaa ili wampe maelekezo, tayari jamaa alikwishasimamisha Prius yake. Aliigongesha kwenye vizuizi vya katikati zinavyozuia pande mbili za barabara, ikasimama, boneti limeharibika lakini hakuumia.
Espen Olsen, msemaji wa Toyota Norway amesema tayari wameshawaita wataalamu wa Toyota kutokea Ubelgiji kuja kuiangalia hiyo gari. Amesema hili ni tukio la kwanza hapa Norway kwa breki za Toyota kushindwa kufanya kazi.
Zaidi kuhusu Toyota angalia marejeo:

No comments:
Post a Comment