Thursday, March 18, 2010

Madina/Oslo

Afukuzwa chuo 

Mohyeldeen Mohammad



Mohyeldeen Mohammad (24) aliyezua balaa hapa Norway kama mwezi mmoja uliopita (bofya kwa marejeo), amefukuzwa toka kwenye chuo cha Kiislamu Madina (Islamic University of Madina), Saudi Arabia, alikokuwa anasoma.

Kijana huyo ameliandikia gazeti la VG kuwapa taarifa hizo na wakili wa kijana huyo, John Christian Elden amethibitisha kuwa mteja wake amefukuzwa chuoni. Mohyeldeen amewaambia VG sababu za kufukuzwa ni za kuchanga masomo na na itikadi kali, kitu ambacho kimeudhi uongozi wa chuo hicho. Amesema amenyang´anywa pasi yake na anasubiri kurudishwa Norway.

Mpaka leo, gazeti la VG limeshindwa kuwapata wanaohusika kwenye chuo hicho, kuhakiki habari za huyo kijana.

Kijana huyo alizua mtafaruku pale aliposema:

”Norway iache kuwadhalilisha Waislamu, vinginevyo kutatokea kama kilichotokea Septemba 11”

Kwenye maandamano yaliyofanywa na Waislamu kama 3000 hivi mjini Oslo, kupinga kitendo cha gazeti la Dagbladet kuchapisha kikatuni kinachomwonyesha Mtume Muhammad (S.A.W) akiwa kama nguruwe.

1 comment:

Anonymous said...

BORA WAMEMTIMUA CHUONI. JAMAA HAJUI VITU ANAJIFANYA MJUAJI. ANATAKA KUTUHARIBIA MAMBO. PAMBAFU!!!