Monday, November 01, 2010

Dakt. Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar 2010 - 2015

Dakt. Ali Mohamed Shein, Rais mteule wa Zanzibar.

Saa 19:00 – 19:300 CET
(21:00 – 21:30 EAT)
Tume ya uchaguzi Zanzibar imetangaza matokeo ya kura za Urais wa Zanzibar. Mgombea wa CCM wa Urais wa Zanzibar, Dakt. Ali Mohamed Shein ameshinda kwa asilimia 50.1% na Maalim Seif Shariff Hamad wa CUF kwa asilimia 49,1% Wagombea wote walikuwa pamoja wakati matokoa yakitangazwa na Maalim Seif amekubali matokeo hayo. Hii inaonyesha kukua na kukomaa kwa demokrasia kwenye visiwa vya Zanzibar na kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kijumla.


National Anthem of Tanzania

Kiswahili Lyrics

Mungu ibariki Afrika
1.
Mungu ibariki Africa
Wabariki Viongozi wake
Hekima Umoja na Amani
Hizi ni ngao zetu
Afrika na watu wake.
Chorus:
Ibariki Afrika
Ibariki Afrika
Tubariki watoto wa Afrika.
2.
Mungu ibariki Tanzania
Dumisha uhuru na Umoja
Wake kwa Waume na Watoto
Mungu Ibariki,
Tanzania na watu wake.
Chorus:
Ibariki Tanzania
Ibariki Tanzania
Tubariki watoto wa Tanzania.


English Translation

God Bless Africa

1.

God Bless Africa.
Bless its leaders.
Let Wisdom Unity and
Peace be the shield of
Africa and its people.

Chorus :

Bless Africa,
Bless Africa,
Bless the children of Africa.

2.

God Bless Tanzania.
Grant eternal Freedom and Unity
To its sons and daughters.
God Bless Tanzania and its People.

Chorus :

Bless Tanzania,
Bless Tanzania,
Bless the children of Tanzania.


6 comments:

Nuhu Kilimanjaro said...

Yaani uzalendo kitu kibaya sanaaa!!!

Kuusoma tu wimbo wa taifa nikajisikia mwili mzima unasisimka, machozi yakataka kunidondoka!!!

Tausi Usi Ame Makame said...

Mimi yalinidondoka!!!

Unknown said...

Mwandishi wa habari hii tafadhali fanya utafiti wa kina ndipo uandike habari. Matokeo ya mshindi wa urais si hayo uliyoyaandika.
Matokeo yalitolewa na Tume ya Uchaguzi zanzibar ni kwamba
Dk. Ali Mohd Shein asilimia 50.1
Maalim Seif Sharif Hamad asilimia 49

Chama Cha Watanzania Oslo said...

Ndg. Alwatan, shukrani kwa taarifa zako. Sisi tumeandika hizi asilimia wakati tukimsikiliza Dakt. Ali Mohamed Shein:

http://www.ustream.tv/channel/bbc-swahili

Kama matokeo ni mengine, tunaomba kumradhi.

Chama Cha Watanzania Oslo said...

Ndg. Alwatan,

unaweza sikiza mwenyewe kwenye kiungo hiki:

http://www.youtube.com/watch?v=pD4YPDVDoCM&feature=player_embedded


Siku njema

Chama Cha Watanzania Oslo said...

Ndg. Alwatan,

Shukran jazeel kwa masahihisho yako. Tutakuwa makini siku zijazo...

Siku njema!