Monday, April 02, 2012

TBC Ikirusha kutangazwa kwa Joshua Nassari Mbunge Mteule Arumeru Mashariki - CHADEMA washindaBaada ya masaa na wasiwasi mwingi hatimaye Mkurugenzi wa Uchaguzi amemtangaza Bw. Joshua Nassari (CHADEMA) kuwa Mbunge mteule baada ya kumshinda Siyoi Sumari wa CCM. Bw. Nassari alitoa mojawapo ya hotuba za kusisimua kutolewa baada ya ushindi. "Tulianza na Mungu, Tutamaliza na Mungu" amesema Mbunge huyo ambaye ni miongoni mwa wabunge vijana zaidi nchini.

1 comment:

MwanaCCM Mdemokrasia wa kweli said...

CCM tukae tukijua kuwa kuna vyama vya upinzani makini sasa si mchezo! Tuliwapeleka wazito wote tukaogopa kumpelekea mwenyekiti wetu Kikwete manaake ingekuwa aibu.

CHADEMA sasa onyesheni upevu angalieni makosa yenu jisahihisheni na nawatakia kila la heri.

Kama alivyosema Nape Mnauye baada ya matokeo kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani.

Wana CCM tukubali tumezidiwa kete na CHADEMA Arumeru.

Tuwe makini na watu kama hawa wanaotukana saa zote. Ikiwezekana tuwaondoe. Kuna vijana wengi CCM wenye uwezo wa kuzungumza bila kutukana!!!

MwanaCCM Mdemokrasia wa kweli