Sunday, May 05, 2013

Utumwa Wa Mihadarati - tatizo la vijana si Kenya tu ni la Afrika Mashariki na sehemu nyingi tu duniani


Kenya imekuwa ikipigana na janga la dawa za kulevya ambazo zinaonekana kuwa kero huku vita dhidi ya dawa hizo vikionekana kutozaa matunda. Wiki moja tu baada ya runinga ya K24 kuangazia kero la dawa hizo huko Mombasa ambapo vijana wanajidunga hata sehemu za siri kwa kukosa mishipa, sasa tumebaini kuwa janga hilo limekolea hadi hapa jijini Nairobi huku vijana ambao wanataka kukoma kuwa waraibu na walanguzi wakikumbwa na changamoto si haba,zikiwemo changamoto za kiafya.

No comments: