Mabadiliko makubwa
ya intaneti yamefanyika
toka ianze kutumika
miaka 40 iliyopita
Mabadiliko makubwa ya intaneti yamefanyika jana, toka ianze kutumika miaka 40 iliyopita, kwenye mkutano mkuu wa shirika la kuthibiti intaneti – ICANN (Internet Corporation for Assigned Names and Numbers, uliofayika mjini Seoul, Korea ya Kusini.
Kuanzia sasa, anwani za mtandao zitakazokuwa na herufi za lugha zingine badala ya kutumia herufi za Kilatini pekee. Hadi sasa herufi zinazokubalika kutengeza majina ya anwani za mitandao ni 26 tu za Kilatini.
Maombi ya kwanza yatakubaliwa kuanzia Novemba 16 mwaka huu. Na ICANN inatarajia kuwa kuanzia katikati ya 2010, anwani za intaneti zenye herufi za lugha zingine zinazoishia kivingine; zitaanza kutumika.
Kwenye mkutano huo mkuu wa ICANN, imekubalika kuwa kuanzia sasa "domeni = domain" hazitakuwa zinaishia tu na ”dot com”, ”dot net”, ”dot org”, n.k.
Watumiaji wa intaneti, wanaweza kutengeza anwani za intaneti zitakazokuwa zinaishia na majina mama wanayotaka, kitu ambacho hadi sasa hakikuwezekana.
Mtu anaweza kujitengenezea tovuti inayoishia kama atakavyo, kama mfano unavyoonyesha hapo chini:
http://www.kipikikusikitishacho.tanzania
http://www.michenzani.zanzibar
http://www.buguruni.shule.ya.msingi. Dar es Salaam
Imeandikwa na mhariri wa blogu